Wateja wanaagiza kutoka mezani. Wahudumu wanapeleka tu.
Mteja anaskani QR ya meza, anaona menyu yako, anaagiza na kulipa kwa simu au cash. Oda inafika bar au jikoni papo hapo, ikiwa na mlio, na mteja anaona dakika za kusubiri.
โฆ
QR kwa kila meza
Kila meza ina QR yake. Oda inajulikana imetoka meza gani, bila kumwita mhudumu.
โฑ
Muda wa kusubiri
Mteja anaona oda yake itachukua dakika ngapi, na muda unapungua kila oda iliyo mbele ikikamilika.
๐
Bar na jikoni kivyake
Kila idara inapokea oda zake kwenye simu, kwa mlio unaojirudia hadi mtu abonyeze "Nimepokea".
๐ต
Simu au cash
Malipo ya simu yanathibitishwa yenyewe. Cash inachukuliwa mezani na mhudumu kabla oda haijatumwa.
๐จ
Chapa yako
Logo, jina, slogan na rangi zako. Mteja anaona biashara yako, si yetu.
๐
Hesabu za zamu
Kila mhudumu ana hesabu yake ya cash. Unaona mauzo, bidhaa zinazouzwa zaidi na kasi ya huduma.